Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, ameuagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuweka mikakati mahususi ya kiutendaji itakayosaidia kuboresha mazingira ya biashara na kukuza ajira nchini. 

Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara ametoa agizo hilo alipokuwa akiwahutubia watumishi wa OSHA katika kikao chao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Shitindi alifafanua kwamba mikakati hiyo inapaswa kujikita katika kuimarisha mifumo ya kiutendaji itakayolenga katika kuboresha huduma zitolewazo kwa wateja na taasisi hiyo ya umma ili kuwaondolea usumbufu watu mbali mbali wanaofanya shughuli mbali mbali za kiuchumi hapa nchini.

“Wakati mwingine tunashindwa kujipanga vizuri katika utekelezaji wa kazi zetu na hivyo kuwasababishia usumbufu mkubwa wateja. Kwa mfano unakuta mkaguzi mmoja wa Usalama na Afya mahali pa kazi anapita katika eneo fulani la kazi asubuhi na mwingine anakuja katika eneo hilo hilo mchana wakati watu hawa wangeweza kufika katika eneo la kazi kwa pamoja na kukamilisha kazi zao za kaguzi kwa wakati mmoja,” alisema Shitindi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza la wafanyakazi mjini Tanga kilichofanyika leo Ijumaa Novemba 24,2017.
Watumishi wa OSHA wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Eric Shitindi, wakati wa kikao chao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Watumishi wa OSHA wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Eric Shitindi, wakati wa kikao chao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya OSHA nje ya ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Mtendaji Mkuu huyo wa Wizara alikuwa Mgeni Rasmi katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa Wakala huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...