THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Awamu Ya Tano Uwanjani By Ngoma Africa Band based in Germany


RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA JENGO LA PSPF PLAZA NA TAWI LA BENKI YA NMB MJINI DODOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na viongozi mbalimbali baada ya kufunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa wafanyakazi wa umma la PSPF Plaza barabara ya Chimwaga mjini Dodoma leo April 23, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na viongozi mbalimbali akiakata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa wafanyakazi wa umma la PSPF Plaza barabara ya Chimwaga mjini  Dodoma leo April 23, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker kuashiria uzinduzi rasmi wa Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage mijini Dodoma leo April 23, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker pamoja na viongozi wengine kukata utepe  kuashiria uzinduzi rasmi wa Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kitengo cha huduma kwa wateja akiwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Gavana Mkuu wa Benki ya Tanzania Dkt. Bernard Kibesse, Mkurugenzi wa Bodi ya NMB Bi. Margareth Ikongo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kuzindua rasmi Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Gavana Mkuu wa Benki ya Tanzania Dkt. Bernard Kibesse, Mkurugenzi wa Bodi ya NMB Bi. Margareth Ikongo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo  na viongozi wengine baada ya kuzindua rasmi Jengo la PSPF Plaza na Makao Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya benki hiyo yaendayo kwa jina la Tawi la Kambarage barabara ya Chimwaga mijini Dodoma leo April 23, 2018. Picha na IKULU


MICHUZI TV: TUKIO ZIMA LA MAZISHI YA MASOGANGE, WIMBO WA BELLE 9 WAZUA GUMZO MSIBANI..


Happy birthday Sensei Fundi Rumadha

I wish you will receive all best things in the world in the coming years, and fulfil all your dreams. Wish you a very happy birthday my Sensei!
- Ankal


BABA WA AGNESS MASOGANGE ASHANGAA KILICHOMUUA MWANAE...


Rais Magufuli Aitaka Bodi ya NMB kuangalia Upya Gawiwo Linalotolewa kwa SerikaliNa: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Bodi ya National Microfinance Bank (NMB) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo kuangali kiasi cha gawiwo kinachotolewa na benki hiyo, kutokana na kiasi hicho kutoongeza ndani ya miaka mitatu mfululizo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati alipokuwa akifungua jengo jipya la Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF) pamoja na tawi jipya la NMB Kambarage lililoko katika jengo hilo.

“Kuna mambo mazuri mengi yaliyofanywa na NMB lakini tunahitaji uhakiki wa gawiwo linalotolewa kwa Serikali, kutokana na gawiwo hilo kutopanda kwa miaka mitatu mfululizo tangu mwaka 2014/2015 mpaka mwaka 2016/2017 ambapo benki hiyo imekuwa ikitoa shilingi Bilioni 16.525 kama gawiwo la hisa ya asilimia 32 iliyonayo katika Benki hiyo,” alisema Rais Magufuli.
Ameendelea kwa kusema, ni matumaini yake kuwa kiasi hicho cha fedha kitapanda kwa mwaka 2017/2018 kutokana na benki hiyo kutengeneza faida kila mwaka. 
Aidha, Rais Magufuli ameipongeza benki ya NMB kwa kuwa na matawi mpaka vijijini pamoja na kutoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 3000 na kutoa misaada ya kijamii ikiwemo madawati 600, kompyuta 300 kwa shule za Sekondari na vitanda vya wagonjwa.
Vilevile Rais Magufuli ameupongeza mfuko wa PSPF kwa kuona fursa ya Serikali kuhamia Dodoma na kujenga jengo ambalo limeboresha na kupendezesha mandhari ya Dodoma ambapo pia ujenzi huo umetoa ajira kwa Watanzania takribani 250.Pia amesema, mfuko huo umekuwa ukitoa mikopo kwa wanachama wake pamoja na kuwekeza katika ujenzi wa viwanda mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanda cha cha Sukari Kagera, kiwanda cha nguo na turubai vilivyopo mkoani Morogoro.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema Rais Magufuli kupitia TAMISEMI ametoa shilingi bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi mbalimbali wa miundombinu mkoani Dodoma.Dkt. Mahenge ametaja miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa stendi mpya ya kisasa yenye uwezo wa kuingia mabasi makubwa 250, magari madogo 600 pamoja na bajaji na bodaboda 300 kwa wakati mmoja.
Aidha, Dkt Mahenge ameitaja miundombinu mingine ambayo ni ujenzi wa soko la kisasa, sehemu ya kupaki malori, miundombinu ya majitaka, maeneo ya kupumzikia pamoja na kuboresha miundombinu ili kuondoa msongamano wa magari.kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji ameutaja mfuko wa PSPF kuwa ndio mfuko wa kwanza kuwekeza katika vitega uchumi Makao Makuu ya Nchi ukiondoa mfuko wa LAPF ambao Makao Makuu yake yapo Mkoani Dodoma.
Jengo la PSPF ni moja ya majengo marefu yaliyoko mkoani Dodoma ambapo ina jumla ya ghorofa 11 pamoja na eneo la maegesho ya magari 161 ambapo mpaka sasa jengo hilo limeshapata wapangaji kwa asilimia 100.


MICHUZI TV: ISRAEL KUSHIRIKI KATIKA MAPINDUZI YA UCHUMI WA VIWANDA NCHINI...


MICHUZI TV: MC PILI PILI AFUNGUKA HAYA KIFO CHA AGNESS MASOGANGE..


Waziri Mhagama ampa Maagizo Msajili wa Vyama vya Siasa Utekelezaji Ripoti ya CAG


TFDA,TBS WAINGIA MAKUBALIANO KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA),imeingia makubaliano ya miaka mitatu na Shirika la Viwango nchini (TBS) katika kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha wajasiriamali na wafanyabiashara wanahudumiwa katika kukuza kazi zao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Agness Kejo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa pamoja kati ya watendaji wa TFDA na TBS,ambapo amesema amesema kuwa changamoto za wafanyabishara na wajasiriamali ni vema zikapatiwa ufumbuzi wake ili watimize malego yao kwa maslahi ya Taifa.

Amefafanua kwenye ujenzi wa viwanda nchini kunategemea mashirika ya TBS na TFDA katika kuviwezesha viwanda nchini kuzalisha bidhaa bora na hatimaye kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje ya nchi.

Amesisitiza hakuna sababu ya mjasiriamali au mfanyabishara kutumia muda mwingi kupata huduma kutoka TBS au TFDA , hivyo ni vema wakashirikiana katika kuondoa changamoto ambazo zipo na huenda zinakwaza wadau hao muhimu katika maendeleo ya nchi

Kejo ameongeza watendaji katika pande mbili hizo ni lazima waendane na azma ya Serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda kuwasaidia afanyabiashara na wajasiriamali kupata elimu kuhusu bidhaa watazozalisha kwa kuzingatia ubora.Aidha amesema ushirikiano huo umefanyika na shirika la Viwango 
Zanzibar ikiwa ni kujenga Tanzania kwa pamoja katika kufikia uchumi wa kati watanzania.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agness Kejo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kati watendaji wa TFDA na TBS katika vituo vya kanda na ipakani kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na taasisi hizo,  jijini Dar es Salaam.
 aimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula  (TFDA), Justin Makisi akizungumza kuhusiana na ufunguzi na mada zitakazojadiliwa katika kufanya kazi kama timu, jijini Dar es Salaam.
03. Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agness Kejo akiwa katika picha ya pamoja watendaji wa TFDA na TBS


ALICHOONGEA MAKONGORO NYERERE WAKATI WA UZINDUZI WA TAWI LA BENKI YA NMB DODOMASHILOLE : "Masogange Atafurahi Kuona nikipika Msibani"


BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 23.04.2018


TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA

Na  Mwandishi Maalum
Tanzania na Israel zimekubaliana kwamba ,  mataifa hayo mawili yana mengi ya kujifunza baina  yao hususani katika eneo la utoaji wa haki na usimamiaji wa sheria.
Hayo yamejiri leo ( jumatatu) wakati Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, alipokutana na kufanya mazungumzo  na Waziri wa Sheria wa Israel Bi. Ayalet Shaked.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Jengo la   Mikutano la Kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere ( JNICC), viongozi hao walikubaliana kwamba kuna haja na umuhimu wa   Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Israel kukutana kwa lengo la kuainisha maeneo ambayo Ofisi hizo mbili  zinaweza kushirikiana.
“  Nadhani  tuna mengi ya  kujifunza kutoka kwenu na halikadhalika nanyi kuna maeneo ambayo   mnaweza kujifunza kutoka kwetu. Hivyo basi, ninaamini kwamba pale itakapowezekana,  kuna umuhimu wa mimi kukutana na mwenzangu ili tuweze kuangalia maeneo ya kipaumbele ambayo tunaweza kubadilishana uzoefu na kupanua wigo wa ushirikiano  baina ya nchi zetu”, akasema Dk. Kilangi.
Akayataja maeneo ambayo  anaamini Tanzania na Israel  zinaweza kushirikiana ni pamoja na  namna bora ya kuimarisha mifumo ya utoaji  haki na ushauri wa kisheria wenye tija, pamoja na eneo la uwezeshwji ( capacity  building).
Mwanasheria Mkuu , Dk. Kilangi  ambaye alifuatana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa  Serikali Bw, Edson Athnas Makallo, aliyatumia mazungumzo  kati yake na Waziri Shaked kuelezea baadhi ya majukumu yake anayoyatekeleza  kama Mshauri Mkuu wa Serikali katika masuala yote yanayohusu sheria pamoja muundo mpya wa Ofisi  ya Mwanasheria Mkuu ambao umehusisha kuanzishwa kwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Kwa upande wake,   Waziri wa Sheria wa Israel, ambaye  Tanzania inakuwa nchi yake ya kwanza kutembelea Barani Afrika, pamoja na kukubaliana na wazo la Dk. Kilangi la kuangalia uwezekano wa  Wanasheria Wakuu kukutana katika muda utakaopangwa. Amesema kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Ofisi nyeti na yenye hadhi ya  juu kabisa katika nchi yoyote ile ikiwamo Israel.
Akaongeza kwamba, majukumu anayoyatekeleza Mwanasheria Mkuu wa  Serikali, Dk. Adelardus Kilangi yanashabihiana na anayotekeleza  Mwanasheria Mkuu wa Israel yakiwamo ya kuisimamia serikali katika  masuala yote yanayohusu sheria, kuiwakilisha serikali katika mahakama za juu na mahakama za chini pamoja na kuendesha mashauri  ya jinai hivyo wawili hao wakipata fursa ya kukutana bila shaka watakuwa na mengi ya kujadiliana na kushirikiana.
Waziri wa Sheria wa Israel Ayalet Shaked anaongoza ujumbe wa  wafanyabiashara kutoka Israel ambao upo hapa nchini kukutana na  wafanyabiashara wa Tanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akiwa katika mazugumzo na  Waziri wa Sheria wa Israel Bi, Aylet Shaked.  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika  katika  Ukumbi wa Mikutano wa Kimatifa wa Julius Nyerere ( JNICC) jijini Dar es Salaam,   viongozi hao walikubaliana kwamba Tanzania na Israel  zinayo maeneo ambayo  kila nchi inaweza kujifunza kutoka kwa mwenzie hususani katika  eneo la utoaji  haki na  usimamiaji wa sheria na kwamba kuna haja  kupitia kwa  Wanasheria  Wakuu wa Serikali wa nchi hizo mbili  kukutana ili  kujadiliana maeneo ya  kushirikiana.   Waziri wa Sheria wa Israel  yupo nchini akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  Dk. Adelardus Kilangi amekutana na kufanya mazugumzo na  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Said Hassan Said. Katika mazungumzo  yao viongozi hao wamebadilishana mawazo  ya namna  ya kushirikiana  katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku  yanayosimamia   masuala ya sheria na utaoaji  haki. Pichani Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bw. Said Hassan Said akimkabidhi Dk. Adelardus Kilangi  Katiba ya Zanzibar ( picha na Ofisi ya AG


HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA LEO APRILI 23, 2018


VOA SWAHILI: Duniani Leo 23rd April 2018


PROFESA MTANZANIA CHUO KIKUU INDIANA APATA TUZO YA WALTON

Beatrice anayefundisha lugha ya Kiswali chuo kikuu cha Massachusetts akimwelezea Profesa Alwiya Omar kabala profesa hyuyo hajapewa tuzo hiyo. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production chini ya udhamini wa Kilimanjaro Studio
Kulia ni Profesa Alwiya Omar ambaye ni Clinical Professor of Linguistics and Afrcan Languages wa chuo kikuu cha jimbo la Indiana akipokea tuzo ya Walton ya ufanisi wa utafiti na ufundishaji wa lugha za kigeni Marekani siku ya Jumamosi April 21, 2018 katika hotel ya Hyatts Regecy, Dulles Virginia.
 Profesa Alwiya Omar akipata picha ya pamoja na maprofesa wenzake wanaofundisha katika vyuo vya Marekani siku ya Jumamosi April 21, 2018 katika hotel ya Hyatts Regecy, Dulles Virginia, siku alipopokea tuzo ya Walton.
Profesa Alwiya Omar akiongea mara baada ya kupokea tuzo hiyo.
Profesa Alwiya Omar akipata picha na wadau
Profesa Alwiya Omar akipata picha na Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV.


MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, MJINI DODOMA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara yake, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati meza kuu) akimsikiliza Mjumbe wa Baraza hilo, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi nchini (TABOA), Enea Mrutu alipokuwa masuala ya usalama barabarani katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara, mjini Dodoma leo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu, akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni (katikati meza kuu), wakati wa kikao cha Baraza hilo lililokua linajadili masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara yake, mjini Dodoma leo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati meza kuu) akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara yake, mjini Dodoma leo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akijibu swali  bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Bungeni mjini Dodoma  Aprili 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) akiteta na Naibu Waziri ,Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Bungeni mjini Dodoma, Aprili23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri M,uu)


ALICHOKISEMA BALOZI WA SERIKALI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA KUHUSU KUDHIBITI MAGONJWA KWA WANANCHI WA PEMBA


UPANDAJI MITI CHUO CHA MAFUNZO YA AMALI MKOKOTONI WAFANA

 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Idirisa Musilimu Hija akizindua zoezi la upandaji Miti Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Idirisa Musilimu Hija akipanda mti baada ya kuzindua zoezi la la upandaji miti Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 MKURUGENZI Mamlaka Mafunzo ya Amali, Bakari Silima akipanda mti katika zoezi la upandaji miti Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja (Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar).
 Maafisa na Wanafunzi mbali mbali  waliojitokeza katika zoezi la upandaji miti lililofanyika Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja  (Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar).


WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA YA MASHARIKI MJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe. Martin Ngoga (watatu kushoto) baada ya mazungumzo, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018. Wengine pichani ni Wabunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, kutoka kushoto ni Dkt. Abdullah Hasnuu Makame, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe. Martin Ngoga, Bungeni mjini Dodoma Aprili 23, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mkono na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe.Martin Ngoga kabla ya mazungumzo yao, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 23, 2018.


TUZO YA MO SALAH YALETA GUMZO

Na Zaynab Nyamka, Globu ya Jamii.

BAADA ya kuchukua tuzo ya mchezajo bora wa Shirikisho ijulikanayo kama PFA Player of the Year akiwa tayari ameshachukua tuzo ya kila mwezi mara tatu katika msimu mmoja na kujiweka rekodi hiyo ndani ya ligi ya EPL nchini Uingereza wadau mbalimbali wameonyesha kukataa kuchukua kwa tuzo hiyo na kumpa nafasi Kelvin De Bruyne.

Mohamed Salah mwenye miaka 25 usiku wa jana aliweza kutangazwa kama mchezaji bora wa shirikisho akiwa amepambanishwa na wachezaji wengine wa EPL na kuwa mchezaji wa saba kutoka Liverpool kuchukua tuzo hiyo.

Hizi ni  takwimu za Mo Salah 

Mohamed Salah - Msimu wa 2017-18 

Ameshiriki mechi: 33
Mikwaju iliyogusa wavu: 64
Magoli: 31
Dakika alizocheza: 2,657
Amechangia magoli: 9
Nafasi alizotoa: 57
Mikwaju: 132
Pasi alizokamilisha: 684

Kwa upande wa De Bruyne mwenye miaka 26 ameweza kutoa mchango mkubwa akichangia magoli 15 na kutoa nafasi za kufunga magoli 104 ikiwa ni zaidi ya mchezaji mwingine katika msimu na kufanikiwa kufunga magoli 8.

Takwimu za De Bruyne.

Kevin de Bruyne - Msimu wa 2017-18 
 Ameshiriki mechi: 34
Mikwaju iliyogusa wavu: 36
Magoli: 8
Dakika alizocheza: 2,836
Amechangia magoli: 15
Nafasi alizotoa: 104
Mikwaju: 84


WADAU WA MAENDELEO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF.


NA. Estom Sanga-

Wadau wa Maendeleo wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kusimamia kwa ufanisi Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- Mpango ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya umaskini kwa Walengwa wake.

Wadau hao wa Maendeleo ambao wamefanya ziara katika maeneo mbalimbali nchini kukutana na Walengwa na kushuhudia namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unavyotekelezwa, wamejionea namna Walengwa wanavyoendelea kuboresha maisha yao kwa kutumia fursa ya kujumuishwa kwenye shughuli za Mpango zilizoanza takribani miaka mitano iliyopita.

Katika maeneo walikotembelea ikiwemo, Zanzibar, Korogwe,Shinyanga,Kagera, na Manyara,wadau hao wa Maendeleo walioambatana na Maafisa wa serikali na wale wa TASAF wameshuhudia mafanikio makubwa katika sekta za elimu, afya,ujenzi wa nyumba ,kilimo ,ufugaji na miradi ya uchimbaji wa malambo ya maji na jitihada mpya za kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana miongoni mwa Walengwa ili kukuza zaidi uwezo wao kiuchumi.

Wadau hao wa Maendeleo pia wamevutiwa zaidi na namna Walengwa wa TASAF walivyoamua kwa hiari yao kutumia sehemu ya ruzuku wanayoipata kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii CHF-na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote wa mwaka katika kaya husika, huku katika maeneo mengi mahudhurio ya watoto wanaotoka kwenye Kaya za Walengwa yamekuwa mazuri ikilinganishwa na kabla ya kuanza kwa shughuli za Mpango.

Kutokana na mabadiliko chanya kwa Walengwa, Kumekuwa na mahitaji makubwa ya Wataalamu hususani wa Ugani ambao wanahitajika kusaidia jitihada za Walengwa hao wa TASAF kutekeleza miradi ya kiuchumi wanayoianzisha ikiwemo ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi, ng’ombe,nguruwe,bata, na kilimo kulingana na maeneo yao.

Aidha imebainika kuwa idadi kubwa ya Wananchi ambao hawakupata fursa ya kuorodheshwa kwenye shughuli za Mpango ,wangelipenda kupata fursa hiyo ili waweze pia kunufaika na huduma zitolewazo kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.Hata hivyo kwa nyakati tofauti Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amezungumzia dhamira njema ya serikali ya kuhakikisha kuwa Wananchi wote wanaostahili kunufaika na shughuli za Mpango wanafanya hivyo nchini kote. Amesema serikali itafanya hivyo pindi fedha zitakapapatikana.

Hii leo Wadau hao wa maendeleo kutoka taasisi zinazochangia utekelezaji wa Mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA zilizoko katika vijiji zaidi ya ELFU TISA sawa na asilimia 70 ya vijiji vyote nchini, wanaendelea na Mkutano wao kwenye Ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama)akijadiliana jambo na Kiongozi wa Shughuli za TASAF Benki ya Dunia Mohammed Muderis kwenye Mkutano wa Wadau.

Baadhi ya Wadau wa Maendeleo wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF . 
Baadhi ya Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa serikali na TASAF wakiwa kwenye Mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaoendela kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.

Mmoja wa Maafisa wa TASAF ,Peter Lwanda aliyeshika kipaza sauti, akiwasilisha taarifa ya ziara ya wadau waliotembelea mkoa wa Shinyanga kuona utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wakifuatilia taarifa inayowasilishwa na mmoja wa Maafisa waliotemebelea maeneo ya utekelezwaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (hayupo pichani). 


Benki ya Barclays Tanzania yasaidia kambi ya upasuaji watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi,yakabidhi kadi za bima ya afya (NHIF) 200 kwa watoto hao.Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy (wa tatu kushoto,) akikabidhi vifaa vya kusaidia upasuaji wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa (wa pili kushoto), katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wengine ni watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.

Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy(kulia), akikabidhi kadi ya bima ya afya (NHIF) kwa mmoja wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi , Joy Jacob katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto (mstari wa nyuma) ni kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa, watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays. Madaktari wa upasuaji wa MOI wakifanya upasuaji mwa mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na tatizo la kichwa kikubwa katika kambi ya upasuaji iliyodhaminiwa na Barclays katika hospitali hiyo jana. Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji wa Mikopo Isiyolipwa wa Barclays Khatibu Mohammedy (nyuma katikati), wakishuhudia.

Baadhi ya watoto 200 waliopewa msaada wa kadi za bima ya afya (NHIF) na benki ya Barclays Tanzania wakionyesha kadi zao katika hafla hiyo katika hafla ambayo benki hiyo pia ilidhamini kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.


SEHEMU YA KWANZA YA HISTORIA YA VITA VYA MAJI MAJI.

Jina la vita vya Maji Maji lilitokana na imani ya matumizi ya “Dawa” iliyochanganywa na maji ,punje za mahindi na mtama zilizosadikika kuwa zitampa mpiganaji kinga ya kutodhurika kwa shambulio la risasi za Wajerumani .Kwa undani wa Historia hii ya Vita vya Maji Maji tizama sehemu ya Kwanza ya Historia ya Vita hivyo.