NA. Estom Sanga-

Wadau wa Maendeleo wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kusimamia kwa ufanisi Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- Mpango ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya umaskini kwa Walengwa wake.

Wadau hao wa Maendeleo ambao wamefanya ziara katika maeneo mbalimbali nchini kukutana na Walengwa na kushuhudia namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unavyotekelezwa, wamejionea namna Walengwa wanavyoendelea kuboresha maisha yao kwa kutumia fursa ya kujumuishwa kwenye shughuli za Mpango zilizoanza takribani miaka mitano iliyopita.

Katika maeneo walikotembelea ikiwemo, Zanzibar, Korogwe,Shinyanga,Kagera, na Manyara,wadau hao wa Maendeleo walioambatana na Maafisa wa serikali na wale wa TASAF wameshuhudia mafanikio makubwa katika sekta za elimu, afya,ujenzi wa nyumba ,kilimo ,ufugaji na miradi ya uchimbaji wa malambo ya maji na jitihada mpya za kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana miongoni mwa Walengwa ili kukuza zaidi uwezo wao kiuchumi.

Wadau hao wa Maendeleo pia wamevutiwa zaidi na namna Walengwa wa TASAF walivyoamua kwa hiari yao kutumia sehemu ya ruzuku wanayoipata kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii CHF-na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote wa mwaka katika kaya husika, huku katika maeneo mengi mahudhurio ya watoto wanaotoka kwenye Kaya za Walengwa yamekuwa mazuri ikilinganishwa na kabla ya kuanza kwa shughuli za Mpango.

Kutokana na mabadiliko chanya kwa Walengwa, Kumekuwa na mahitaji makubwa ya Wataalamu hususani wa Ugani ambao wanahitajika kusaidia jitihada za Walengwa hao wa TASAF kutekeleza miradi ya kiuchumi wanayoianzisha ikiwemo ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi, ng’ombe,nguruwe,bata, na kilimo kulingana na maeneo yao.

Aidha imebainika kuwa idadi kubwa ya Wananchi ambao hawakupata fursa ya kuorodheshwa kwenye shughuli za Mpango ,wangelipenda kupata fursa hiyo ili waweze pia kunufaika na huduma zitolewazo kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.Hata hivyo kwa nyakati tofauti Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga amezungumzia dhamira njema ya serikali ya kuhakikisha kuwa Wananchi wote wanaostahili kunufaika na shughuli za Mpango wanafanya hivyo nchini kote. Amesema serikali itafanya hivyo pindi fedha zitakapapatikana.

Hii leo Wadau hao wa maendeleo kutoka taasisi zinazochangia utekelezaji wa Mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA zilizoko katika vijiji zaidi ya ELFU TISA sawa na asilimia 70 ya vijiji vyote nchini, wanaendelea na Mkutano wao kwenye Ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama)akijadiliana jambo na Kiongozi wa Shughuli za TASAF Benki ya Dunia Mohammed Muderis kwenye Mkutano wa Wadau.

Baadhi ya Wadau wa Maendeleo wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF . 
Baadhi ya Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa serikali na TASAF wakiwa kwenye Mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaoendela kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.

Mmoja wa Maafisa wa TASAF ,Peter Lwanda aliyeshika kipaza sauti, akiwasilisha taarifa ya ziara ya wadau waliotembelea mkoa wa Shinyanga kuona utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 
Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wakifuatilia taarifa inayowasilishwa na mmoja wa Maafisa waliotemebelea maeneo ya utekelezwaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (hayupo pichani). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...