Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA),imeingia makubaliano ya miaka mitatu na Shirika la Viwango nchini (TBS) katika kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha wajasiriamali na wafanyabiashara wanahudumiwa katika kukuza kazi zao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Agnes Kijo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa pamoja kati ya watendaji wa TFDA na TBS,ambapo amesema amesema kuwa changamoto za wafanyabishara na wajasiriamali ni vema zikapatiwa ufumbuzi wake ili watimize malego yao kwa maslahi ya Taifa.

Amefafanua kwenye ujenzi wa viwanda nchini kunategemea mashirika ya TBS na TFDA katika kuviwezesha viwanda nchini kuzalisha bidhaa bora na hatimaye kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje ya nchi.

Amesisitiza hakuna sababu ya mjasiriamali au mfanyabishara kutumia muda mwingi kupata huduma kutoka TBS au TFDA , hivyo ni vema wakashirikiana katika kuondoa changamoto ambazo zipo na huenda zinakwaza wadau hao muhimu katika maendeleo ya nchi

Kijo ameongeza watendaji katika pande mbili hizo ni lazima waendane na azma ya Serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda kuwasaidia afanyabiashara na wajasiriamali kupata elimu kuhusu bidhaa watazozalisha kwa kuzingatia ubora.Aidha amesema ushirikiano huo umefanyika na shirika la Viwango 
Zanzibar ikiwa ni kujenga Tanzania kwa pamoja katika kufikia uchumi wa kati watanzania.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agnes Kijo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kati watendaji wa TFDA na TBS katika vituo vya kanda na ipakani kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na taasisi hizo,  jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula  (TFDA), Justin Makisi akizungumza kuhusiana na ufunguzi na mada zitakazojadiliwa katika kufanya kazi kama timu, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Agnes Kijo akiwa katika picha ya pamoja watendaji wa TFDA na TBS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...