Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde leo amekabidhi mashine mbalimbali kwa wajasiriamali wa vikundi 31 na kuwataka kuhakikisha wanazitumia kwa kujiongezea kipato na kuenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa Viwanda.

Akizungumza na wanavikundi hao na wakazi wa Dodoma, Mavunde amesema mashine hizo zimenunuliwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo na kwamba dhamira yake ni kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi kwa kubadili maisha yao.

“Leo Tumegawa mashine hizi mkazitumie zibadilishe maisha yenu msizifungie stoo zikajaa vumbi na msipozitumia kwa malengo yaliyokusudiwa hamuwezi kufikia malengo yenu,Mashine hizi zikaunge mkono falsafa ya Rais ya uanzishaji wa viwanda ili kufikia uchumi wa viwanda,”amesema Mavunde

Hata hivyo amewahakikisha kuwa amejipanga kuhakikisha anawakwamua wananchi wake kiuchumi kupitia fursa mbalimbali na kwamba anakuja na mradi wa kuchimba mabwawa ya kufugia samaki.

“Kuna teknolojia imekuja ya kufuga samaki ambayo unaweza kufuga nyumbani, hiyo ndo mipango ya ofisi ya Mbunge ya kuwawezesha wananchi kiuchumi na pia kwa upande wa kilimo nimetafuta wataalamu kutoka India tunaangalia eneo la Nzasa kulitumia kwa majaribio ya kilimo cha mboga mboga na ufugaji samaki,”amesema
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani katika hafla ya kukabidhi mashine mbalimbali kwa vikundi vya wajasiriamali.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa wajasiriamali.
Mashine zilizokabidhiwa kwa vikundi vya wajasiriamali


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...