Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bibi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wamefanya ziara katika migodi ya Mpipiti pamoja na Sekenke iliyopo katika Wilaya ya Singida vijijini na Wilaya ya Iramba, mkoani Singida.

Dhumuni ni ziara hiyo ni kujifunza na kuangalia kwa ukaribu jinsi Wachimbaji hao wanavyofanya shughuli zao za kila siku hususan katika suala zima la mazingira. Wakiwa aktika ziara hiyo waliongea na Viongozi wa Wachimbaji hao wadogo na kujionea shughuli hizo za uchimbaji katika migodi hiyo zinavyokwenda. Viongozi hao wa Wachimbaji walitoa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika uchimbaji ikiwemo miundombinu mibovu , umeme na garama za ukodishaji wa mashine za kuvutia maji(pampu) na kompresa.

Kabla ya kuanza ziara hiyo ujumbe huo ulipata nafasi ya kumtembelea Katibu YTawala wa Moa wa Singida Dkt. Angela Mageni Lutandula Ofisini kwake na kujitambulisha na kumweleza dhumuni la safari yao mkoani humo. Akiongea Katibu Tawala aliwakaribisha Wajumbe hao mkoani Singida na kuwasititiza wakajionee wao wenyewe shughuli hizo za uChimbaji wa madini kwa Wachimbaji wadogowadogo mkoani kwake.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi (katikati) akiongea na ujumbe wa Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais walipomtembelea Ofisini kwake kwenda kujitambulisha kabla ya kuanza ziara ya kutembelea Wachimbaji wadogo wadogo katik Mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga(wa mwisho kushoto) toka Ofisi ya Makamu wa Rais wakipata maelezo jinsi Wachimbaji wadogo wanavyoingia kwenye mashimo kwa kutumia kamba kutoka kwa Kiongozi wa Mgodi wa Wachimbaji wadogo wa Mpipiti katika Wilaya ya Singida Vijijini Bwana Geston Ali.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga akiangalia jinsi dhahabu inavyochujwa kutolewa katika udongo kwa kutumia maji katika mgodi mdogo wa Mpipiti uliopo wilaya ya Singida Vijijini.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji (katikati) , Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga pamoja na Afisa Afya Mazingira Bi Suzan Nchala wakionyeshwa na Bwana Athman Mrisho (Mkurugenzi wa mgodi) jiwe linakuwa kabla ya kuingizwa kwenye mashine kwa kuvunjwavunjwa katika mgodi mdogo wa Sekenke wilayani Iramba mkoani Singida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...