KITUO cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC kimezinduwa mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, yaani Kinondoni na Ubungo.

Akizungumza na wadau wa mradi huo yaani baadhi ya wasaidizi wa sheria, maofisa ustawi wa jamii, wanasheria, mahakimu, Askari Polisi Dawati la Jinsia, maofisa watendaji wa mitaa kutoka wilaya za Kinondoni na Ubungo, Mwenyekiti wa CRC, Saida Mukhi aliwataka wadau hao kushirikiana ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinakomeshwa na kupungua.

Alisema lengo la mradi huo unaofadhiliwa na shirika la Legal Service Facilities (LSF) ni kuhimarisha zaidi upatikanaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Aliongeza kuwa mradi huo utajikita zaidi katika utoaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa waathirika na kuhakikisha mfumo wa upatikanaji wa haki unafanya kazi vizuri.

“…wadau katika maeneo hayo mnatakiwa kuhakikisha tunapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na wahusika kunyimwa uhuru,” alisema Bi. Saida Mukhi akifungua warsha ya wadau hao.

Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo akifafanua zaidi kwa washiriki wa semina hiyo alisema mradi huo utaendeshwa katika Kata za Makumbusho na Kawe kwa Wilaya ya Kinondoni huku kwa Wilaya ya Ubungo utajikita kwenye Kata ya Saranga.

Alisema CRC itashirikiana na wadau katika maeneo hayo kuhakikisha inapiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vimekuwa na madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii na mara nyingine kuwanyima uhuru.
Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni na Ubungo. Kulia ni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo.Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Ofisa Mradi wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Suzan Charles akitoa ufafanua juu ya mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam.Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi akichangia mada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...