NA EVELYN MKOKOI

Katika hali isiyoya kawaida, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amefanya ziara ya Oparesheni maalum kwa kushirikiana na jeshi la Police kitengo cha FFU ili kuweza kubaini uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa uchimbani na uchotaji wa mchanga katika vyanzo vya maji na maeneo mengine.

Akiwa katikati ya Mto Mpigi uliopo katika mpaka wa Dar es salaam na Bagamoyo usiku wa kuamkia leo, naibu Waziri Mpina alisema kuwa watu wanaochimba na kuchota mchanga kiholelea watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria, kutaifishwa kwa magari yao na hata kufikishwa mahakamani.

“kama mnavyoona hapa na kama tulivyosikia kutoka kwa mtu wa DAWASA haya mabomba ya maji yanayopita katika mito yanaharibika kutokana na shughuli hizi na serikali inaweza kuingia gharama kubwa sana kurekebisha mabomba haya kama bomba hili Mtaalam amesema hapa itagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 kutengeneza bomba hili.” Alisema Mpina.

Aidha Mpina alisema ukiachilia mbali uharibifu wa Miundo Mbinu hiyo ya Maji pamoja na Mazingira wananchi wnaweza pia kukosa maji kwa takribani muda wa wiki mbili.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwa na mchanga mkononi akiwasikiliza maafisa wataalam katikati Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni katibu wake Bw. Daniel Sagata, na kulia ni Afisa kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenge akieleza kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kati kati ya mto Mpigi katika eneo la Mpaka wa Bagamoyo na Dar es Salaam, ambapo uharibifu huo Umeharibu eneo ambapo limepita Bomba kubwa la maji safi (halipo pichani) linalo safirisha maji kutoka Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini na kuhudunia seheu ya mkoa mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, Bomba ambalo lipo hatarini kuharibika.
Afisa Mtaalam kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenje (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Sehemu ya mto Mpigi ( haipo Pichani, iliyoharibiwa vibaya kutokana na shughuli za uchimbaji wa mchanga. (Picha na Evelyn Mkokoi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...