MBUNGE wa Ilala,Mussa Azzan Zungu ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kujengea nyumba za wasanii wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA).
Akizungumza wakati wa kufunga tamasha la siku mbili lililowakutanisha wasanii zaidi ya 600 kutoka vikundi mbalimbali vikiwemo vya Tanzania One Theatre (TOT)Zungu alisema ametoa saruji hiyo ili kuwasaidia SHIWATA kuendeleza juhudi za kuwakomboa wasanii kwa kuwajengea makazi.
Mbunge Zungu pamoja ya kushuhudia michezo mbalimbali alishindwa kujizuia kuungana na wasanii kucheza na kutunza ngoma ya asili ya Sangura kutoka kabila la Wapogoro mkoani Morogoro.
>Bendi za muziki wa dansi za Hisia Sound ya Abdul Salvador,bendi ya TOT na Umoja Sound ziliwakonga wasanii na wengine waliohudhuria tamasha hilo.
Katika tamasha hilo lililofunguliwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza wasanii wa fani mbalimbali walionesha vipaji vyao vya kucheza sarakasi,ngoma za asili,maigizo,muziki wa dansi,muziki wa asili na taarabu.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ambae tamasha hilo awali lilikuwa lifanyike kijiji cha Wasanii  Mkuranga na baadaye kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kutokana na mvua ya msimu uliopita kuharibu barabara ya kwenda kijijini alisema jutihada zifanyike ili mwakani lifanyike  Mkuranga.
> > > > >
Mkurugenzi wa TOT,Gasper Tumaini alisema tamasha hilo limefana na wao wako tayari kushirikiana na SHIWATA katika matamasha mengine.

Pamoja ya kudhaminiwa na Kampuni ya SBC inayotengeneza soda za Pepsi, Kampuni ya Simu ya TTCL kulikuwa na msaada wa kisheria wa kujikinga na magonjwa ya UKIMWI.
 Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey Mngereza akiwa na Mkurugenzi wa TOT,Gasper Tumaini.
 Wasanii wa Kikundi cha Kaole wakimkaribisha Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey Mngereza katika tamasha la SHIWATA.
 Msanii maarufu nchini,Bakari Mbelemba (Mzee Jangala) na wageni wengine akifuatilia kwa karibu maonesho ya wasanii.
 Washiriki wa tamasha wakifuatilia kwa karibu maonesho ya wasanii.
 Wasanii wa Kaole wakicheza ngoma mbele ya wageni waalikwa.
Mbunge Zungu akituza  kikundi cha ngoma za asili cha Sangura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...