Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya barabara na majengo katika halmashauri zote nchini kuzingatia mikataba ya ujenzi, huku akiwaonya tabia ya kuchelewesha kukamilisha miradi kwa wakati.

Jafo aliyasema hayo katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya barabara na madaraja wilayani Kisarawe.Amesema Ofisi ya Rais, Tamisemi haitofumbia macho wakandarasi ambao wameshinda tenda za ujenzi na kuonesha uwezo mdogo.

“Pia hatutafumbia macho ucheleweshaji wa miradi bila sababu yeyote ya msingi kinyume na matarajio yaliyoainishwa ndani ya mkataba,”amesema Jafo.

Naibu Waziri Jafo katika ziara zake hivi karibuni ikiwemo ujenzi wa daraja la Twangoma lililopo wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam amekuwa akisisitiza wakandarasi kuzingatia ubora wa madaraja yanayojengwa  nchini ili yaweze kudumu kwa muda mrefu. 

Jafo amemaliza ziara yake leo wilayani Kisarawe na anatarajia kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro, Songwe, Njombe, Singida, Tabora, Kagera, Mwanza na Mara.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wataalam wa ujenzi wa daraja la Kologombe linalounganisha Kijiji cha Gwata na Dololo wilayani Kisarawe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za mji wa Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelekezo kuhusu ujenzi wa barabara ya kisarawe mjini kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri Mbena.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Kologombe wilayani Kisarawe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...